Manchester, England
Mchezaji wa Manchester City, Benjamin Mendy amekutwa hana hatia katika makosa sita ya ubakaji na moja la udhalilishaji kijinsia aliyokuwa akidaiwa kuwafanyia wasichana wanne.
Katika kesi hiyo iliyokuwa ikisikilizwa Ijumaa hii katika mahakama ya Chester Crown, mshirika wa Mendy, Louis Saha Matturie naye amekosekana na hatia katika makosa matatu ya ubakaji yaliyokuwa yakimkabili dhidi ya wasichana wawili.
Mendy na mshirika wake, Matturie wamekuwa wakikabiliwa na tuhuma za kuwabaka wasichana matukio ambayo ilielezwa kwamba yalikuwa yakifanyika nyumbani kwa Mendy Prestbury, Cheshire na katika nyumba moja ya ghorofa iliyopo jijini Manchester.
Mendy alikuwa ameziba sura yake kwa mikono yote miwili wakati mahakama ikimtamkia kwamba hana hatia katika makosa sita kwenye kesi ambayo imechukua takriban miezi sita sasa ambapo Mendy alikuwa akituhumiwa kwa kuwalaghai wasichana na kuwatumia kujiridhisha kijinsia.
Baada ya uamuzi huo kutolewa wakili mmoja wa utetezi alisema kwamba ingawa kesi hiyo ilihusisha pesa, mapenzi na watu maarufu ilijaa vituko na mwishowe watuhumiwa wamekutwa hawana hatia.
Kwa mara ya kwanza Mendy alikamatwa Novemba 2020 na Agosti mwaka alifunguliwa mashtaka ya ubakaji ambayo awali yalihusisha wasichana 13 na hatimaye alisimamishwa na klabu yake kutokana na tuhuma za kubaka zilizokuwa zikimkabili.
Kocha wa Man Ciy, Pep Guardiola aliwahi kumzungumzia mchezaji huyo na kesi hiyo akisema kwamba anamjua Mendy kuwa ni mchezaji mahiri na muungwana lakini hajui mambo aliyokuwa akiyafanya akiwa kwake.
Kwa upande wake wakili mmoja wa Mendy alinukuliwa akisema amefurahi kwa mteja wake kufutiwa tuhuma za kubaka wasichana wanne na sasa anaangalia suala zima la kufutiwa tuhuma nyingine mbili ili aweze kuyajenga upya maisha yake.
Kimataifa Mendy ‘achomoka’ kesi ya ubakaji
Mendy ‘achomoka’ kesi ya ubakaji
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
