Copenhagen, Denmark
Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola amempongeza straika wake, Erling Haaland akisema kuwa ni mmoja wa mastraika bora aliofanya nao kazi na namba za mabao za mchezaji huyo zinazungumza.
Pep ambaye juzi Jumanne alimuweka benchi Haaland kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya FC Copenhagen iliyoisha kwa sare ya bila kufungana, alisema mchezaji huyo kutoka Norway ameweza kuendeleza moto alioanza nao katika soka England.
Haaland hadi sasa amefunga mabao 15 kati ya 33 yaliyofungwa na timu yake katika Ligi Kuu England, idadi ambayo inakaribia nusu ya mabao yote ya timu hiyo lakini rekodi hiyo pia inapambwa na hat trick (mabao matatu mechi moja) tatu, hapo hapo ana rekodi ya kufunga mabao mengine saba katika Ligi ya Mabingwa Ulaya na michuano mengine.
“Ni kati ya mstraika bora, nimekuwa na mastraika wengi wazuri na Erling ni mmoja wao, anaelewa kwa haraka na ni mtu mzuri, ana uwezo wa kuifanyia mambo timu yake lakini tunahitaji kufanya kazi pamoja na hicho ndicho kinachotokea, nazungumza mno kuhusu yeye lakini wakati mwingine sitakiwi kufanya hivyo kwa sababu namba zinazungumza,” alisema Pep.
Wiki iliyopita Haaland alifunga mabao mawili wakati Man City ikiibuka na ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya FC Copenhagen lakini timu hizo ziliporudiana Jumanne Man City ikiwa ugenini, Pep aliamua kumpumzisha pamoja na baadhi ya wachezaji wengine muhimu kwa kile ambacho kocha huyo alidai kwamba mchezaji huyo na wengine walikuwa wakiandamwa na uchovu.
Kimataifa Pep: Haaland straika wangu bora
Pep: Haaland straika wangu bora
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
