London, England
Katika mkakati wa kuhakikisha inamsajili mshambuliaji, Harry Kane, klabu ya Bayern Munich ipo tayari kuvunja rekodi yake ya Pauni 68 milioni ilizotoa kumsajili beki Mfaransa, Lucas Hernandez.
Kane ambaye pia anawindwa na PSG na klabu kadhaa kubwa za Ulaya, ameweka wazi nia ya kutaka kuondoka Tottenham Hotspur ili kusaka changamoto kwingineko Ulaya huku Bayern ikiwa chaguo lake la kwanza.
Mpango wa Spurs kumuuza Kane upo wazi ingawa klabu hiyo inataka kupiga pesa ndefu na Bayern wameonekana kuwa wagumu katika hilo wakati PSG inayojiandaa kumuuza mshambuliaji wake, Kylian Mbappe huenda ikaingia katika mbio hizo baada ya kumuuza Mbappe.
Habari za ndani kutoka Spurs zinadai kwamba klabu hiyo pamoja na kutoonesha haraka ya kumuuza Kane lakini inazisubiri kwa hamu pesa za mauzo ya mchezaji huyo izitumie kukiongezea nguvu kikosi chake.
Miongoni mwa wachezaji ambao Spurs inawawinda kwa kutegemea mauzo ya Kane ni pamoja na kiungo wa Barcelona, Franck Kassie ambaye pia ni mchezaji wa kimataifa wa Ivory Coast.
Wengine ni beki Mfaransa, Clement Lenglet na mshambuliaji wa Nottingham Forest, Bernna Johnson ambaye thamani yake inatajwa kufikia Pauni 50 milioni.
Kimataifa Bayern kuvunja rekodi kwa Kane
Bayern kuvunja rekodi kwa Kane
Read also