Na mwandishi wetu
Klabu ya Yanga imeendelea kutambulisha safu yao mpya ya kazi baada ya kutangaza uteuzi wa mchambuzi wa soka wa Azam Media, Ali Kamwe kuwa ofisa habari mpya wa klabu hiyo.
Kamwe mbali na Azam Media pia amewahi kufanya kazi katika Kampuni ya New Habari akiwa mmoja wa waandishi na wachambuzi kwenye gazeti la Dimba, hata hivyo kwa sasa kampuni ya New Habari wamesimamisha uzalishaji.
Utambulisho wa Kamwe umekwenda sambamba na utambulisho wa mchambuzi wa soka, Priva Abiud kuwa Msimamizi Mkuu wa Kitengo cha Digitali na Maudhui, utambulisho huo umekuja baada ya leo mchana klabu hiyo kumtambulisha mtendaji mkuu wao mpya, Mzambia Andre Mtine na kuzindua tovuti mpya na program tumishi ya Yanga.
Huo ni mwendelezo wa upangaji wa safu mpya ya uongozi na vitengo mbalimbali vya timu hiyo tangu kuingia kwa uongozi mpya wa Rais wa klabu hiyo, Hersi Said aliyeingia madarakani Julai 9 mwaka huu akichukua mikoba ya Dk Mshindo Msolla.
Ali Kamwe amechukua nafasi iliyoachwa wazi na Hassan Bumbuli ambaye ilielezwa kuwa amemaliza mkataba wake na Wanajangwani hao, mkataba uliodumu kwa kipindi cha miaka mitatu.
Soka Ali Kamwe ofisa habari mpya Yanga
Ali Kamwe ofisa habari mpya Yanga
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
