Na mwandishi wetu
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk Pindi Chana anatarajiwa kufungua mashindano ya Judo Afrika Mashariki yatakayoanza kesho Jumamosi kwenye viwanja vya Don Bosco, Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Chama cha Judo Tanzania (JATA) Innocent Mallya amesema kwamba tayari timu za Uganda, Zanzibar, Rwanda na Burundi zimeshawasili nchini ambapo zitaungana na wenyeji Tanzania kufikisha jumla ya timu tano.
Kwa mujibu wa Mallya, maandalizi ya mashindano hayo yamekamilika na kuwataka mashabiki na watu wote wanaopenda mchezo huo kujitokeza kushuhudia bure kwa lengo la kujifunza.
“Mambo yameshaiva, mashindano yanaanza kesho, tunawahimiza watoto, wakubwa na wadau wa michezo kwa ujumla waje washuhudie burudani, hakuna kiingilio ni sehemu ya kujifunza,”alisema.
Mallya alisema itapendeza kama mashabiki watajitokeza waione timu yao ya Taifa ikipigania ushindi ambao mara ya mwisho waliupata mwaka 2018.
Bingwa mtetezi wa mashindano hayo ni Kenya aliyeshinda mwaka jana kwenye michuano iliyofanyika Uganda wakati Tanzania ikishika nafasi ya pili na Burundi ya tatu.
Akifafanua kuhusu mashindano hayo Mallya alisema yatasaidia katika maandalizi ya timu ya Taifa kwa ajili kushriki mashindano mbalimbali ya Afrika na Dunia pamoja na kufuzu Michezo ya Olimpiki.
Sports Mix Dk Chana kufungua mashindano ya judo
Dk Chana kufungua mashindano ya judo
Read also