Na mwandishi wetu
Kocha mkuu wa Azam FC, Youssouf Dabo amesema ushindi walioupata Jumapili hii dhidi ya Dodoma Jiji umewaongezea ari ya kupambana kuwania ubingwa wa Ligi Kuu NBC Tanzania.
Katika mchezo huo, Azam iliibuka na ushindi wa mabao 4-1 na kufikisha pointi 43 sawa na vinara Yanga, lakini matajiri hao wameendelea kubaki nafasi ya pili kutokana na kuzidiwa idadi ya mabao ya kufunga.
“Nawapongeza vijana wangu kwa kufuata vizuri kile nilichowaelekeza kwenye mazoezi, ushindi umetuongezea ari ya kupambana kurudi kileleni na kubeba ubingwa wa ligi kuu msimu huu,” alisema Dabo.
Naye kocha mkuu wa Dodoma, Francis Baraza alisema makosa yaliyofanywa na mabeki wake ndiyo yaliyosababisha wapoteze mchezo huo ambao awali walikuwa na matarajio ya kuondoka angalau na pointi moja.
“Naweza kusema mabao yote manne waliyotufunga tumewapa, mabeki wangu wamejichanganya na kuwapa nafasi washambuliaji wa Azam kutuadhibu, tunakubali haya matokeo na tunarudi kujipanga ili kufanya vizuri mechi zinazofuata,” alisema Baraza.
Soka Ushindi waamsha ari Azam
Ushindi waamsha ari Azam
Read also