London, England
Dhamira ya kuifanya Tottenham Hotspur timu shindani katika Ligi Kuu England na Ulaya inaendelea na leo imemsaini kiungo, Yves Bissouma kwa ada ya Pauni 25 milioni kutoka Brighton & Hove Albion.
Kiungo huyo mkabaji wa Mali mwenye miaka 25 anakuwa mchezaji wa tatu kusajiliwa Spurs baada ya wengine wawili kusajiliwa mapema mwezi huu ambao ni Ivan Perisic na kipa Fraser Forster.
Bissouma alikuwa pia akiwaniwa na klabu ya Aston Villa ambao ofa yao ilikataliwa mwezi Januari mwaka huu kama ilivyokuwa kwa Everton na Arsenal na keshokutwa anatarajia kufanyiwa vipimo vya afya kabla ya kuanza rasmi kuitumikia Spurs kwa ajili ya msimu wa 2022/23.
Spurs tangu mwaka 2018 walikuwa wakimfuatilia Bissouma wakati huo akiwa mchezaji wa Lille ya Ufaransa na alikuwa kwenye orodha ya wachezaji waliowindwa kwa ajili ya kuchukua nafasi ya Moussa Dembele lakini wakabadili uamuzi kwa kumsajili Tanguy Ndombele wa Lyon na Bissouma akajiunga na Brighton kwa ada ya Pauni 15 milioni na kuonyesha uwezo mkubwa akiwa na timu hiyo.
Kocha mkuu wa Spurs, Antonio Conte alionekana kuvutiwa zaidi na kiwango cha Bissouma hasa katika mechi dhidi yao msimu uliopita na tangu hapo inadaiwa amekuwa akifuatilia kwa karibu maendeleo ya mchezaji huyo na hatimaye amefanikiwa kumpata.
Mabosi wa Spurs inadaiwa wamemuhakikishia fedha Conte kwa ajili ya kujenga timu ya ushindani kwa ajili ya msimu ujao hasa baada ya kuvutiwa na ushindani aliouonyesha msimu uliopita ambapo timu hiyoilimaliza ligi ikiwa nafasi ya nne nyuma ya Man City, Liverpool na Chelsea huku ikiwaacha vigogo wengine wa England, Arsenal na Man United katika nafasi ya tano na sita.
Kimataifa Spurs yasajili kifaa cha tatu
Spurs yasajili kifaa cha tatu
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
