Na mwandishi wetu
Mfungaji Bora wa Ligi Kuu ya NBC msimu uliopita, George Mpole ameelezwa kujiunga na timu ya FC St-Éloi Lupopo ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwa mkataba wa miaka miwili.
Mshambuliaji huyo ametajwa kukamilisha dili hilo na Lupopo baada ya kuachana na Geita Gold hivi karibuni, ambayo aliichezea kwa msimu mmoja na kuibuka mfungaji bora wa Ligi Kuu kwa kufunga mabao 17 na kutwaa kiatu hicho mbele ya Fiston Mayele wa Yanga aliyefunga mabao 16.
Meneja wa Mpole, Karim Helasi, amekaririwa akisema kuwa kiwango alichoonyesha Mpole msimu uliopita ndicho kilichowavutia Lupopo na kuhitaji saini yake huku akiamini ataenda kuwa na muendelezo mzuri kwenye Ligi Kuu ya Congo maarufu kama Ligue 1.
“Mpole ni mchezaji mzuri ambaye timu yoyote ingehitaji kuwa naye lakini tunachoangalia sasa ni maslahi na mahala pa kazi, naamini FC Lupopo ni mahala sahihi kwake,” alisema Helasi
Mpole naye alinukuliwa akisema kuwa huu ni wakati wa kutafuta changamoto mpya mahala pengine baada ya kucheza soka nchini Zambia na Tanzania kwa muda mrefu hivyo ni wakati wa kubadili mazingira ya kazi ingawa anafahamu ugumu uliopo lakini atapambana.
Soka Mpole atimkia FC Lupopo
Mpole atimkia FC Lupopo
Read also