Na mwandishi wetu
Klabu ya Namungo leo Ijumaa imetangaza kumsajili kiungo wa kati, Frank Domayo ‘Chumvi’ kwa ajili ya kukiongezea nguvu kikosi hicho kuelekea duru la lala salama la Ligi Kuu NBC.
Domayo aliyewahi kuwika akiwa na JKT Ruvu kabla ya kutua Yanga na kisha kuitumikia Azam FC kwa miaka minane, amesajiliwa na timu hiyo baada ya kukaa nusu msimu bila timu tangu alipoachana na Azam msimu uliopita.
Namungo imemtambulisha kiungo huyo wa zamani wa timu ya taifa, Taifa Stars kupitia mitandao yake ya kijamii ikionesha namna gani imefurahishwa na ujio wa mchezaji huyo.
Tayari Domayo ameshaanza mazoezi na kikosi hicho cha mkoani Lindi kinachojiandaa vikali jijini Dar es Salaam kabla ya jana kuanza safari ya kuelekea Tanga kuvaana na Coastal Union kwenye mechi itakayopigwa Januari Mosi, mwakani kwenye Uwanja wa Mkwakani.
Huo unakuwa usajili wa kwanza kwa Namungo katika dirisha hili dogo la usajili lililofunguliwa Desemba 16 likitarajiwa kufungwa Januari 15, mwakani.
Soka Domayo amwaga wino Namungo
Domayo amwaga wino Namungo
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
