Buenos Aires, Argentina
Mshambuliaji wa zamani wa timu ya taifa ya Argentina, Carlos Tevez (pichani) amelazwa hospitali mjini hapa akisumbuliwa na maumivu ya kwenye kifua.
Tevez, 40, ambaye pia amewahi kuzichezea klabu za Man United, Man City na West Ham za England na Boca Junior ya Argentina, kwa sasa ni kocha wa timu Independiente inayoshiriki Ligi Kuu Argentina.
Taarifa ya Independiente kupitia mtandao wa X (Twitter) hata hivyo ilieleza kuwa vipimo vilionesha kuwa Tevez hakuwa katika hali mbaya ingawa atalazimika kuendelea kukaa hospitali kama njia ya kuchukua tahadhari.
Tevez ambaye ameichezea timu ya taifa ya Argentina mara 76 kuanzia mwaka 2004 hadi 2015, alikabidhiwa majukumu ya kuinoa Independiente Agosti mwaka jana ingawa kabla ya hapo alikuwa akiinoa timu ya Rosario Central.
Akiwa England, Tevez amewahi kutwaa mataji ya ligi kuu mara tatu, mara mbili akiwa na Man United katika msimu wa 2007-08 na 2008-09 na mwaka 2011-12 alibeba taji hilo akiwa na Man City.
Kimataifa Carlos Tevez alazwa hospitali
Carlos Tevez alazwa hospitali
Related posts
Read also