Na mwandishi wetu
Winga wa Simba, Peter Banda ameeleza kuwa anaedelea vizuri akitarajia kuwa fiti kwa mechi kuanzia wiki ijayo huku akisisitiza anatamani kuipambania Simba kwenye mechi baada ya kutofanya hivyo takriban miezi mitatu sasa.
Banda alikuwa akiuguza jeraha la kifundo cha mguu alilolipata walipokuwa wakiumana na Singida BS Novemba 9, mwaka jana ambapo alitolewa nje kipindi cha pili dakika chache baada ya kufunga bao katika mechi hiyo iliyoisha kwa sare ya 1-1.
Ikiwa ni siku tatu zimepita tangu aanze mazoezi rasmi, Banda alisema anajisikia vizuri, hasikii maumivu na anazidi kuimarika hali inayompa moyo mpaka wiki ijayo atakuwa fiti kwa asilimia 100.
“Kwa sasa naendelea vizuri sana, nafurahi nimerudi tena maana ni muda mrefu kama miezi mitatu hivi, natamani kuipigania tena Simba kwenye mechi na sasa niko fiti kama asilimia 70 hivi nafikiri mpaka wiki ijayo nitakuwa fiti kwa asilimia 100, nitakuwa tayari kabisa,” alisema Banda.
Mbali na Banda, wachezaji wengine waliorejea Simba hivi karibuni kutoka majeruhi ni mshambuliaji Moses Phiri na beki Henock Inonga waliozidi kuongeza upana wa kikosi hicho kuelekea mechi za Ligi Kuu NBC na Ligi ya Mabingwa Afrika.
Soka Banda ajipa matumaini
Banda ajipa matumaini
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
