Na mwandishi wetu
Uongozi wa timu ya Dodoma Jiji umeanza mchakato wa kumsaka kocha mkuu mpya wa kukinoa kikosi chao kinachoshiriki Ligi Kuu NBC baada ya kuachana na Melis Medo (pichani).
Uongozi huo kupitia tamko lake la leo Jumanne kwenye kuraza zao za mitandao ya kijamii umeeleza kuachana na Medo ili kumpa nafasi ya kushughulika na changamoto za kifamilia zinazomkabili.
Katibu Mkuu wa Dodoma Jiji, Fortunatus Johnson alisema: “Tumeachana na Medo kwa makubaliano ya pande zote mbili, tumefanya hivyo kumpa nafasi aweze kumaliza matatizo ya kifamilia ambayo yanamkabili kiasi cha kushindwa kutimiza majukumu yake ya kikazi.”
Johnson alisema tayari mchakato wa kumsaka kocha mpya atakayerithi mikoba ya Medo raia wa Marekani, umeanza na watahakikisha wanaharakisha jambo hilo ili kumpata kocha wa kukiongoza kikosi chao katika mechi za ligi zinazoendelea hivi sasa.
Alisema tayari wameshaanza kupokea CV za makocha kadhaa kutoka ndani na nje ya nchi na wataendelea hivyo hadi mwisho wa wiki hii, baada ya hapo watazichambua na kumpata kocha bora atakayekinoa kikosi hicho.
Soka Dodoma Jiji yasaka kocha mpya
Dodoma Jiji yasaka kocha mpya
Read also