Miami, Marekani
England imeshika nafasi ya tatu kwenye fainali za Kombe la Dunia 2026 ikiilaza Ufaransa mabao 6-4 huku Jude Bellingham akiweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza wa timu hiyo kufunga mabao saba katika moja ya Kombe la Dunia.
Timu hizo ziliumana katika mechi ya kusaka mshindi wa tatu Jumamosi Julai 18, 2026 huku mechi ya fainali kati ya Hispania na Argentina ikisubiriwa kupigwa Jumapili Julai 19, 2026.
Bellingham ambaye pia ni kiungo wa Real Madrid, awali alifungana na nahodha na mshambuliaji wa England, Harry Kane aliyefunga mabao sita katika fainali za Kombe la Dunia 2018 nchini Urusi.
Rekodi kama hiyo ya mabao sita kabla ya hapo ilikuwa ikishikiliwa na Garry Lineker aliyeifungia England idadi mabao kama hiyo ya mabao kwenye fainali za Kombe la Dunia 1986 nchini Mexico.
Katika mechi dhidi ya Ufaransa, Bellingham, 23, aliingizwa uwanjani dakika ya 79 na kufunga bao lililotokana na shambulizi la kushtukiza.
Dakika 12 kabla ya hapo alikuwa afunge bao kwa mkwaju wa penalti lakini akaamua kumpa nafasi hiyo Bukayo Saka ambaye hakumuangusha, aliitumia vyema penalti hiyo kuipatia England bao.
Saka hata hivyo baada ya mechi alisema kwamba ni Bellingham ndiye aliyemwambia aende akapige mpira huo wa penalti ili apate hat trick (mabao matatu).
Katika mechi hiyo mbali na Bellingham, mabao mengine ya England yalifungwa na Declan Rice dakika ya tatu, Konsa dakika ya 18 na Saka ambaye alifunga dakika za 37, 45 na 87.
Mabao ya Ufaransa yalifungwa na Kylian Mbappe aliyefunga mawili dakika za 48 na 66 wakati mengine mawili yalifungwa na Barcola dakika ya 54 na Dembele dakika ya 90.
Kimataifa England yashika nafasi ya tatu
England yashika nafasi ya tatu
Read also
