Manchester, England
Klabu ya PSG imepata mpinzani katika mbio zake za kuiwania saini ya mshambuliaji wa Napoli, Victor Osimhen ambaye habari zimeibuka kwamba anawindwa pia na Man United.
Chanzo kimoja cha habari kimearifu kuwa Osimhen, 25, ambaye pia ni mchezaji bora Afrika, ametokea kuwa tishio katika kuzifumania nyavu akiwa na Napoli jambo ambalo limezishawishi klabu kadhaa kuisaka saini yake.
Katika wiki za hivi karibuni, PSG ilihusishwa na mipango ya kumtaka mshambuliaji huyo ikiamini ni mchezaji sahihi kuziba nafasi ya Kylian Mbappe ambaye ameshatangaza nia yake ya kuondoka katika klabu hiyo baada ya msimu huu.
Kocha wa PSG, Luis Enrique ameshasema kuwa timu yake inatakiwa ifikirie maisha bila ya Mbappe na ameanza kulifanyia kazi jambo hilo kwa kumuweka benchi mchezaji huyo katika mechi zao za hivi karibuni.
PSG japo inataka Mbappe abaki lakini inatambua nia ya mchezaji huyo kutaka changamoto mpya hivyo inaamini inaweza kumkosa hasa kwa namna anavyoonesha utayari wa kutaka kuondoka huku jina lake likitajwa zaidi katika klabu ya Real Madrid.
Kwa kuutambua ukweli huo PSG mbali na kocha wake kuanza kujipanga bila ya Mbappe lakini klabu hiyo pia imeshaanza kumsaka mshambuliaji wa kuziba pengo hilo na Osimhen anatajwa kuwa chaguo namba moja.
Man United ambayo mambo yake hayako vizuri msimu huu nayo ipo katika mkakati wa kujiimarisha kwa ajili ya msimu ujao na inadaiwa Osimhen ni kati ya wachezaji waliomo katika mpango huo ambao ni sehemu ya juhudi za mwekezaji mpya wa klabu hiyo, bilionea wa Uingereza Sir Jim Ratcliffe.
Kimataifa Man United, PSG zamgombea Osimhen
Man United, PSG zamgombea Osimhen
Read also