Manchester, England
Straika wa Man City, Erling Haaland huenda akajikuta matatani kwa kumshutumu kwenye mitandao ya kijamii mwamuzi Simon Hoper aliyechezesha mechi yao na Tottenham iliyoisha kwa sare ya mabao 3-3.
Haaland alikerwa na Hoper kwa uamuzi aliouchukua katika dakika tano za nyongeza kwa kupuliza filimbi ya faulo aliyochezewa licha ya mchezaji huyo kuuwahi mpira.
Tukio hilo katika mechi ya jana Jumapili lilimkera Haaland na wachezaji kadhaa wa Man City waliomzonga mwamuzi huyo hata baada ya mechi lakini kwa Haaland hakuishia katika kumzonga mwamuzi uwanjani pekee.
Baada ya hapo mchezaji huyo alikwenda kwenye mtandao wa X (zamani Twitter) na kuandika neno ‘Wtf’ ambalo ni lugha ya mtaani ya kumdhalilisha mtu.
Hoper hata hivyo alijichanganya kwani baada ya tukio hilo alionekana kama aliyeruhusu mchezo uendelee kabla ya kupuliza filimbi akiwapa Man City mpira wa adhabu jambo ambalo ilikuwa kama kuwarudisha nyuma badala ya kupewa ‘advantage’.
Uamuzi huo ambao City wanaona kama umewanyima nafasi ya kupata bao na kutoka na pointi tatu muhimu katika Ligi Kuu England (EPL), mbali na kupingwa na wachezaji, pia ulikosolewa na baadhi ya wachambuzi.
Kocha wa Man City, Pep Guardiola alipoulizwa na waandishi wa habari kuhusu tukio hilo alijibu kwa kifupi, “swali jingine? Siwezi kutoa maoni kama ya Mikel Arteta.”
Arteta ambaye ni kocha wa Arsenal, kwa sasa yuko matatani na huenda akaabidhiwa kwa kauli aliyoitoa baada ya mwamuzi kuipa bao Newcastle wakati ikiumana na Arsenal, Arteta aliuita uamuzi huo kuwa ni fedheha na aibu katika EPL.
Matokeo ya EPL kwa mechi za mwishoni mwa wiki…
Bournemouth 2-2 Aston Villa
Chelsea 3-2 Brighton
Liverpool 4-3 Fulham
West Ham 1-1 Crystal Palace
Man City 3-3 Tottenham
Arsenal 2-1 Wolverhampton
Brentford 3-1 Luton Town
Burnley 5-0 Sheffield United
Nottingham Forest 0-1 Everton
Newcastle 1-0 Man United
Kimataifa Haaland amchamba mwamuzi mitandaoni
Haaland amchamba mwamuzi mitandaoni
Read also