Milan, Italia
Klabu ya Lecce ya Italia imemfuta kazi kocha wake, Roberto D’Aversa (pichani) baada ya kocha huyo kumpiga kichwa mshambuliaji wa Verona, Thomas Henry katika mechi ya Serie A ambayo Lecce ililala kwa bao 1-0.
D’Aversa, 48, na Henry kila mmoja alipewa kadi nyekundu baada ya tukio hilo ambalo lilitokana na mzozo ulioibuka mara baada ya mwamuzi kumaliza mchezo.
Akizungumza na waandishi wa habari baadaye, D’Aversa alikiri mwenyewe kwamba kosa alilolifanya halisameheki na siku moja baada ya mechi hiyo iliyochezwa Jumapili uongozi ulitangaza kumfuta kazi.
Klabu ya Lecce ilieleza kwa kifupi kuwa uamuzi wa kumfuta kazi kocha huyo ulitokana na tukio lililojitokeza baada ya mechi.
Kipigo hicho kinaifaya Lecce kushuka hadi nafasi ya 15 kwenye Ligi Kuu Italia maarufu Serie A ikiwa nafasi mbili nyuma ya Verona na hivyo kulisogelea janga la kushuka daraja.
Mambo kwa ujumla si mazuri kwa klabu ya Lecce kwenye Serie A kwa kuwa hadi sasa imeshinda mechi moja tu kati ya 12 za ligi hiyo kubwa nchini Italia ikiwa imepoteza tisa kati ya hizo na nyingine kutoa sare.
D’Aversa ambaye amewahi kuzinoa timu za Virtus Lanciano, Parma na Sampdoria alikabidhiwa jukumu la kuinoa timu hiyo majira ya kiangazi mwaka jana akichukua nafasi ya Marco Baroni.
Kimataifa Kocha atimuliwa kwa kumpiga kichwa mchezaji
Kocha atimuliwa kwa kumpiga kichwa mchezaji
Read also