Na mwandishi wetu
Bondia Japhet Kaseba amesema kuwa hana mpango wa kuwashawishi watoto wake wacheze mchezo huo na wala hatamuunga mkono mtoto wake yeyote kujiingiza katika mchezo huo.
Kaseba ambaye awali alitamba kwenye ‘kick-boxer’ kabla ya baadaye kuingia rasmi kwenye ngumi amesema hiyo inatokana na mazingira magumu yaliyokuwepo kwenye mchezo huo kabla ya hivi karibuni Serikali kuonekana kutilia mkazo kwenye michezo yote kwa ujumla.
“Sitamani wala siwezi kumshawishi mwanangu yeyote kuingia katika mchezo huu kutokana na mazingira yenyewe halisi ya namna ya kutaka kufanikiwa kupitia ngumi, siyo mazingira rafiki ndiyo maana hata mimi sikuwa nashawishika kuwaweka watoto wangu huko.
“Lakini anagalau sasa Serikali inaonekana kutilia mkazo kwenye haya masuala ya ngumi na michezo yote kwa ujumla, kasi iliyopo sasa na namna mazingira ya mchezo husika yanavyoandaliwa inatia moyo na pengine tunaweza kuanza kupiga hatua,” alisema Kaseba.
Aliongeza kuwa kwa sasa watoto wake wamekazania zaidi kusoma, mwingine akiwa yupo chuo kwa sasa na aliwakazania wanawe kwenye mrengo huo ili wapate mazingira bora ya maisha yao ya baadaye kuliko kuingia kwenye ngumi mapema kabla ya kujenga misingi yao imara baadaye.
Ngumi Kaseba: Sitaki wanangu wawe mabondia
Kaseba: Sitaki wanangu wawe mabondia
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
