Madrid, Hispania
Kiungo wa zamani wa Man City na timu ya Taifa ya Hispania, David Silva amekutwa na hatia ya kumpiga mwanamke na mahakama imemtoza faini ya dola 1000 kwa kumuumiza mwanamke huyo.
Taarifa za mahakama moja ya Hispania zilieleza kuwa tukio hilo lilitokea Juni 19 katika tamasha la Carnaval kwenye Kisiwa cha Canary ambapo vurugu zilitokea kati ya kundi la Silva na la watu wengine ambapo katika vurugu hizo Silva alimzuru mwanamke huyo.
Baada ya kutokea vurugu, Silva anadaiwa kumshika kwa nguvu mwanamke huyo na kumsukuma hali ambayo ilimfanya aanguke na kuumia, mgongo, goti na kupata michubuko kwenye kiwiko cha mkono na hivyo kulazimika kupatiwa matibabu.
Watu wengine wawili nao walikutwa na hatia ya kushambulia, mmoja alitozwa faini wakati mwingine alitozwa faini pamoja na kuhukumiwa kwenda jela kwa miezi minane.
Silva aliyetamba na Man City na kubeba mataji manne ya Ligi Kuu England, tangu mwaka 2020 amekuwa akiichezea klabu ya Real Sociedad ya Hispania na alikuwamo katika kikosi cha Hispania kilichobeba Kombe la Dunia mwaka 2010 nchini Afrika Kusini.
Kimataifa David Silva apiga mwanamke, atozwa faini
David Silva apiga mwanamke, atozwa faini
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
