Valencia, Hispania
Mshambuliaji wa Man United anayecheza kwa mkopo katika klabu ya Barcelona, Marcus Rashford ameendelea kudhihirisha ubora wake baada ya kufunga bao timu hiyo ikitoka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Elche.
Katika mechi hiyo ya La Liga iliyochezwa Jumamosi Januari 31, 2026, ushindi wake umeifanya Barcelona au Bara kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa La Liga kwa tofauti ya pointi nne.
Barca ambao ni mabingwa watetezi wa La Liga walikuwa wa kwanza kupata bao lililofungwa na Lamine Yamal baada ya kuinasa pasi ya Dani Olmo kabla ya kumzunguka kipa wa Elche, Inaki Pena na kuujaza mpira wavuni lango likiwa wazi.
Elche hata hivyo walipambana na kupata bao la kusawazisha dakika ya 28 mfungaji akiwa Alvaro Rodriguez lakini dakika 11 baadaye, Barca waliongeza bao la pili lililofungwa na Ferran Torres na kuzifanya timu ziende mapumziko Barca wakiwa mbele kwa mabao 2-1.
Rashford aliyekuwa benchi alipewa nafasi ya kuingia kipindi cha pili na kuipatia Barca bao la tatu kwa mpira uliotokana na krosi ya Yamal.
Hilo linakuwa bao la 10 kwa Rashford msimu huu, hapo kabla mchezaji huyo aliifungia Barca bao katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi FC Copenhagen, Jumatano iliyopita.
Kimataifa Rashford atupia Barca ikishinda 3-1
Rashford atupia Barca ikishinda 3-1
Read also
