Na mwandishi wetu
Kinara wa mabao Simba, Moses Phiri anatarajiwa kukaa nje kwa muda wa wiki mbili kufuatia majibu ya vipimo alivyofanyiwa juzi vya MRI na X-ray.
Mshambuliaji huyo aliumia Jumatano iliyopita wakati timu yake ikicheza na Kagera Sugar kwenye mchezo wa Ligi Kuu NBC ambapo timu hizo zilitoka sare ya kufungana bao 1-1 kwenye Uwanja wa Kaitaba, Bukoba.
Daktari wa Simba, Edwin Kagabo alieleza leo kuwa mchezaji huyo atalazimika kukaa nje wiki mbili kutokana na maumivu hayo ambayo hata hivyo siyo makubwa sana.
“Majibu yanaonesha jeraha alilolipata Phiri siyo kubwa sana lakini anapaswa kuwa chini ya uangalizi ili kupona haraka sababu ni mchezaji muhimu kwenye kikosi chetu kulingana na mashindano yanayotukabili,” alisema Kagabo.
Daktari huyo ameeleza kuwa yeye na jopo la madaktari wenzake watapambana kuhakikisha Phiri anarudi uwanjani haraka kabla ya kuanza kwa mechi za makundi za Ligi ya Mabingwa Afrika.
Phiri atakosa mechi mbili za kufungia mwaka 2022 dhidi ya KMC itakayopigwa Jumatatu ijayo na ule wa Desemba 30 dhidi ya Tanzania Prisons.
Soka Phiri nje wiki mbili
Phiri nje wiki mbili
Read also