Barcelona, Hispania
Mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Brazil, Neymar ameieleza mahakama jana Jumanne kuwa hakushiriki mazungumzo ya mkataba wake kutoka Santos kwenda Barcelona badala yake alisaini kile alichoambiwa na baba yake.
Neymar alijiunga na Barcelona mwaka 2013 akitokea Santos, amefikishwa mahakamani na kampuni inahojihusisha na uwekezaji ya DIS akikabiliwa na tuhuma za ubadhirifu na rushwa, tuhuma ambazo amezikana pamoja na watuhumiwa wengine wanane.
DIS inadai kumiliki asilimia 40 ya haki za mchezaji huyo, katika malalamiko yake inadai kupoteza haki zake katika usajili wa mchezaji huyo kwa kuwa thamani yake ilishushwa.
“Baba yangu wakati wote ndiye aliyekuwa akisimamia jambo hili, sikushiriki katika mazungumzo, nilisaini kila kitu baba alichoniambia,” alisema Neymar ambaye kwa sasa ana miaka 30 na kuongeza kuwa kuchezea klabu ya Barcelona wakati wote ilikuwa ndoto yake ya utotoni.
Washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni wazazi wa Neymar, klabu za Barcelona na Santos, marais wa zamani wa Barcelona, Josep Maria Bartomeu na Sandro Rosell pamoja na rais wa zamani wa klabu ya Santos, Odilio Rodrigues.
Naye baba mzazi wa mchezaji huyo, Neymar da Silva Santos wakati akijitetea aliiambia mahakama, “Lengo letu lilikuwa kuandaa maisha yake ya soka Ulaya, tayari mwenyewe alishajitengenezea maisha hayo na alijua ndoto yake ya kuichezea Barcelona, tulisaini mkataba wa wale waliokuwa chaguo lake la kwanza.”
Katika madai yao, DIS wanataka Neymar afungwe miaka mitano jela wakati waendesha mashtaka Hispania wanataka afungwe miaka miwili na faini ya Euro 10 milioni lakini pia wanataka Rosell afungwe jela miaka mitano na Barcelona ipigwe faini ya Euro 8.4 milioni.
Rais wa klabu ya Real Madrid, Florentino Perez ambaye aliitwa kutoa ushahidi alisema kwamba klabu yake ilitoa kitita cha Euro 45 milioni mwaka 2011 na Euro 36 milioni mwaka 2013 ili kumsajili Neymar lakini mchezaji huyo aliamua kujiunga na Barcelona.
Awali wakili anayewatetea Neymar na wenzake alisema kwamba mchezaji huyo hakufanya kosa lolote la kijinai na kuongeza kuwa mahakama za Hispania hazina haki ya kuishitaki familia ya Neymar kwa kuwa kosa hilo lilifanyika Brazil, nchi ambayo matukio ya aina hiyo hayana adhab
Kimataifa Neymar aanza kujitetea mahakamani
Neymar aanza kujitetea mahakamani
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
