Na mwandishi wetu
Kocha Mkuu wa Namungo FC, Denis Kitambi amepanga kuongeza wachezaji wanne kwenye dirisha dogo ili kukirudisha kikosi chake kwenye mbio za kuwania ubingwa wa Ligi Kuu NBC na michuano ya Kombe la FA.
Kocha huyo amezitaja nafasi ambazo anahitaji kuziimarisha ni ushambuliaji kwa kunasa wachezaji wawili, kiungo mchezeshaji mmoja na beki wa kati mmoja.
“Uongozi umeshatenga fungu kwa ajili ya usajili huo, nafurahi sababu naamini kikosi changu kitakuwa kimeimarika tofauti na ilivyo sasa,” alisema Kitambi ambaye hivi karibuni amechukua nafasi ya Hanour Janza raia wa Zambia.
Kitambi ameeleza kuwa pamoja na kikosi chake kutopewa nafasi kubwa ya ushindi lakini malengo yake ni kuhakikisha wanamaliza ligi hata kwenye nafasi tano za juu ifikapo mwishoni mwa msimu.
Baada ya kuifunga Ihefu FC juzi, Namungo sasa inashika nafasi ya nane kwenye msimamo wa ligi ikikusanya pointi 22 katika michezo 17.
Soka Kitambi kusajili wanne Namungo
Kitambi kusajili wanne Namungo
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
