London, England
Baada ya kuchapwa mabao 6-2 na Tottenham, kocha wa Leicester City, Brendan Rodgers hajakata tamaa badala yake amesema ataendelea kupambana japo anatambua kibarua chake kinamulikwa.
Leicester au The Foxes kwa sasa wanashika mkia katika Ligi Kuu England wakiwa na pointi moja tu ambayo waliipata katika mechi moja kati ya mechi saba tangu kuanza kwa ligi hiyo, hayo yakiwa ni matokeo mabaya kwa timu hiyo tangu mwaka 1983.
“Naielewa hali hii, wakati wote nilikuwa mwenye kuamini kwamba tutaivuka, sijaiona timu ambayo imekosa hali ya kujiamini, hiyo wakati wote ni ishara nzuri, nitaendelea kupigana wakati wote lakini naelewa hali ya matokeo ilivyo, kushindwa mechi sita mfululizo si jambo zuri kwa yeyote,” alisema Rodgers.
“Kwa hali yoyote ile nitaendelea kuwapa heshima wamiliki kwa sababu wamekuwa wakinipa ushirikiano mkubwa, chochote kitakachonitokea mimi hapa Leicester kama nitabaki nitaendelea kupambana, wakati wote nitakuwa mwenye kuwashukuru wamiliki,” alisema.
“Watu wataangalia matokeo na kuona ni 6-2 na nafikiri watashangaa na kusema Leicester imefanyiwa maangamizi tena, kwangu hilo halinisumbui, kipindi cha kwanza ilikuwa ni kama ile Leicester tunayoijua na kikosi cha Brendan Rodgers kilichofanya miaka michache iliyopita, tuliwasumbua na kupeleka mashambulizi tukatengeneza nafasi lakini mwisho wa yote ni ngumu kukubali kilichotokea,” alisema.
“Wachezaji nao wanatakiwa kubeba sehemu ya lawama, si Rodgers pekee, ni kwa pamoja si kocha tu, tulikuwa 11 pale na katika siku za karibuni tumekuwa si wenye kupata mafanikio,” aliongeza.
Kimataifa Rodgers hajaikatia tamaa Leicester
Rodgers hajaikatia tamaa Leicester
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
