London, England
Klabu ya soka ya Chelsea inajipanga kumsajili nahodha wa zamani wa Arsenal, Pierre-Emerick Aubameyang ambaye kwa sasa anaichezea Barcelona.
Mpango huo ukifanikiwa itakuwa ni kumrudisha mshambuliaji huyo kwenye Ligi Kuu England baada ya kuondoka Arsenal takriban miezi saba iliyopita na kujiunga na Barcelona akiwa mchezaji huru baada ya kutokea tofauti kati yake na kocha Mikel Arteta wa Arsenal.
Kocha wa Chelsea, Thomas Tuchel ndiye anayedaiwa kutoa ushawishi wa kumsajili mchezaji huyo akitaka kuungana naye kwa mara nyingine baada ya kuwa pamoja Borussia Dortmund na anaamini atasaidia kuimarisha safu ya ushambuliaji ya timu hiyo.
Baada ya kumsajili Raheem Sterling kutoka Man City na kuondoka kwa Romelu Lukaku, Chelsea haijasajili mshambuliaji wa hadhi na hivyo Aubameyang ametajwa kuwa mtu sahihi katika safu ya ushambuliaji ya timu hiyo.
Nguvu ya kumsajili mchezaji huyo pia inachangiwa na tajiri wa klabu hiyo, Todd Boehly ambaye vyombo vya habari vinaripoti kuwa jina la Aubameyang pia limejadiliwa mbele ya tajiri huyo.
Aubameyang mwenye miaka 33 sasa, huenda asiwe na tabu ya kurudi England hasa baada ya Barcelona kumsajili Robert Lewandowski kutoka Bayern Munich na hivyo klabu hiyo huenda isiwe na tatizo la kumuachia mchezaji huyo kama mazungumzo yatakwenda vizuri.
Msimu wa 2021/22 ambao ameukuta nusu akiwa Barcelona, Aubameyang, nyota wa zamani wa timu ya Taifa ya Gabon, amefunga mabao 13 katika mechi 23, rekodi ambayo si mbaya kwa mshambuliaji ambaye amecheza nusu ya msimu.
Kimataifa Chelsea yamgeukia Aubameyang
Chelsea yamgeukia Aubameyang
Read also
