Na mwandishi wetu
Timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars imeondoka jioni ya leo kuelekea nchini Niger kwa ajili ya kucheza mechi ya kwanza ya kuwania kufuzu kushiriki michuano ya Afcon, mwakani.
Kikosi hicho kilichoambatana na Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia kama mkuu wa msafara kinatarajiwa kuwasili Niger majira ya saa nne usiku ambapo ni sawa na saa sita usiku ya Tanzania.
Timu hiyo imesafiri na kikosi cha wachezaji 26 huku kocha wa timu hiyo, Kim Polsen akisisitiza kuhitaji ushindi kuelekea kwenye mchezo huo utakaopigwa Jumamosi hii kwenye Uwanja wa Jenerali Kerekou ili kujiweka sawa na kupata nguvu kwa ajili ya mechi yao ya pili dhidi ya Algeria itakayopigwa Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam mnamo Julai 8, mwaka huu.
Timu nyingine iliyo Kundi F na Stars kuwania kushiriki michuano hiyo itakayofanyika nchini Ivory Coast ni Uganda.
Stars inawania kushiriki michuano hiyo baada ya kuikosa michuano iliyopita iliyofanyika nchini Cameroon na Senegal kutawazwa kuwa bingwa. Mara ya mwisho Stars kushiriki Afcon ilikuwa mwaka 2019 ambapo ilitolewa mapema kwenye hatua ya makundi.
Soka Stars yaifuata Niger
Stars yaifuata Niger
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
