Na mwandishi wetu
Azam FC imeshindwa kuutumia vyema uwanja wake wa nyumbani baada ya kutoka sare ya 0-0 na Simba katika mechi ya Ligi Kuu NBC iliyochezwa Jumapili, Aprili 5, 2028 kwenye dimba la Azam Complex, Dar es Salaam.
Matokeo hayo yanaibakisha Simba katika nafasi ya pili ikiwa na pointi 35 baada ya kucheza mechi 16 wakati Azam ikibaki katika nafasi ya tatu na pointi zake 33 ikiwa imecheza mechi 17.
Azam iliuanza vizuri mchezo ikitawala kwa muda mrefu wa kipindi cha kwanz lakini haikuweza kufanya shambulizi lililozaaa matunda katika lango la Simba.
Kipindi cha pili, Simba nao walianza kuonesha uhai wakidhibiti mashambulizi ya Azam na kutengeneza nafasi kadhaa lakini walishindwa kumtungua kipa wao wa zamani, Aishi Manula.
Katika mechi nyingine ya ligi hiyo, TRA United wakiwa nyumbani Sheikh Amri Abeid walitoka na ushindi wa mabao dhidi ya Singida Black Stars.
Kimataifa Simba, Azam zagawana pointi
Simba, Azam zagawana pointi
Related posts
Read also
