Na mwandishi wetu
Kocha Mkuu wa Timu za Taifa za Soka za Wanawake, Bakari Shime amesema anaamini timu ya U-20 ya Tanzanite Queens itafuzu Kombe la Dunia, katika michezo miwili dhidi ya Djibouti inayotarajiwa kuchezwa hapa nchini.
Shime alisema michezo yote miwili dhidi ya Djibouti itachezwa Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam Oktoba 8 kabla ya kurudiana Oktoba 11, mwaka huu.
“Tuna faida ya kucheza nyumbani michezo yote miwili kwa sababu Djibouti wamechagua kucheza hapa nchini mechi yao, naamini tutashinda michezo yote miwili,” alisema Shime.
Alisema anaamini kikosi chake kwa sababu kinaundwa na nyota waliocheza Kombe la Dunia la Wanawake chini ya miaka 17 nchini India.
Baada ya mchezo dhidi ya Djibouti, Tanzanite Queens itakuwa imebakisha mchezo mmoja dhidi ya Nigeria na endapo itafanikiwa kuitoa Nigeria, itafuzu Kombe la Dunia linalotarajiwa kufanyika nchini Colombia, mwakani.