Vaduz, Liechtenstein
Cristiano Ronaldo ameendelea kuwa mshambuliaji tegemeo wa timu ya taifa baada ya kufunga bao wakati Ureno ikiichapa Liechtenstein mabao 2-0 katika mechi ya kufuzu Kombe la Ulaya 2024 ‘Euro 2024’.
Kwa kufunga bao hilo Ronaldo mwenye umri wa miaka 38 sasa anakuwa amefikisha jumla ya mabao 128 na timu yake ya Taifa na hajaonesha dalili zozote za kutaka kustaafu kuichezea timu hiyo.
Ureno ambayo tayari imejikatia tiketi ya kucheza fainali hizo mwakani nchini Ujerumani, bao lake la pili katika mechi hiyo lilifungwa na Joao Cancelo katika dakika ya 57.
Ronaldo ambaye kwa sasa anacheza Saudi Arabia ameendelea kuwa teheme
Timu nyingine ambayo imeibuka na ushindi katika mechi za kufuzu Euro 2024 ni Slovakia ambayo imeichapa Iceland mabao 4-2 na hivyo kufuzu moja moja ikiwa Kundi J nyuma ya Ureno.
Matokeo mechi za kufuzu Euro 2024 zilizochezwa Alhamisi…
Cyprus 1-3 Hispania
Georgia 2-2 Scotland
Liechtenstein 0-2 Ureno
Azerbaijan 3-0 Sweden
Estonia 0-2 Austria
Bulgaria 2-2 Hungary
Luxembourg 4-1 Bos-Herze
Slovakia 4-2 Iceland
Montenegro 2-0 Lithuania
Kimataifa Ronaldo aipaisha Ureno
Ronaldo aipaisha Ureno
Read also