Na mwandishi wetu
Simba leo Jumatano imeichapa Singida Fountain Gate mabao 2-0 katika mechi ya Kombe la Mapinduzi iliyochezwa kwenye dimba la Amaan Complex mjini Unguja.
Simba ilianza kuhesabu bao lake la kwanza dakika ya 47 mfungaji akiwa Willy Onana kwa mpira wa adhabu ambao aliupiga kiufundi kutokea upande wa kushoto wa lango la Singida na kumshinda kipa Ibrahim Rashid Parapanda.
Miquissone aliwainua vitini mashabiki wa Simba katika dakika ya 59 baada ya kufunga bao akiunganisha pasi ya Shomary Kapombe iliyotokea upande wa kulia.
Baada ya kuinasa pasi hiyo nje kidogo ya eneo la 18, Miquissone alionesha umahiri wake kwa kuunganisha shuti la moja kwa moja ambalo pia lilimshinda, Parapanda.
Katika mechi nyingine ya Kombe la Mapinduzi iliyochezwa leo, APR iliilaza JKU mabao 3-1 huku mabao ya washindi yakifungwa na Niyibizi Ramadhan aliyefunga mawili na Mbaoma Victor wakati bao pekee la JKU likifungwa na Saleh Masoud.
Soka Simba yaichapa Singida 2-0
Simba yaichapa Singida 2-0
Read also