London, England
Mshambuliaji wa Manchester City, Erling Haaland ametwaa tuzo ya mwanasoka bora wa mwaka wa Chama cha Wanasoka Profesheno (PFA), tuzo aliyokabidhiwa Jumanne hii usiku.
Haaland alikuwa na msimu mzuri wa 2022-23 akifunga mabao 52 katika mechi 53 za mashindano tofauti na kuiwezesha City kubeba taji la Ligi Kuu England (EPL), FA na Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Mshambuliaji huyo mwenye miaka 23, hadi kutwaa tuzo hiyo, amewashinda nyota wenzake wa Man City, Kevin de Bruyne na John Stones na Martin Odegaard na Bukayo Saka wa Arsenal pamoja na mshambuliaji wa zamani wa Tottenham Harry Kane ambaye kwa sasa anaichezea Bayern Munich.
Tuzo hiyo ni mwanzo mzuri kwa Haaland katika msimu huu wa 2023-24 akiwa ametoka kutwaa tuzo ya mwanasoka bora wa msimu wa EPL kwa wanaume, tuzo aliyopewa mwezi Mei na Chama cha Waandishi wa Soka England.
Katika tuzo ya PFA, Saka wa Arsenal yeye alitwaa tuzo ya mwaka ya Young Player ikiwa ni mara ya kwanza kufanya hivyo baada ya kuingia katika kinyang’anyiro hicho kwa mara nne mfululizo.
Kwa upande wa wanawake tuzo ya PFA imechukuliwa na mshambuliaji wa Aston Villa, Rachel Daly ambaye pia ndiye aliyemaliza msimu uliopita akiwa mfungaji bora wa ligi ya wanawake akiwa na mabao 22 wakati tuzo ya mwaka ya Young Player imechukuliwa na Lauren James wa Chelsea.
Kimataifa Haaland abeba tuzo ya PFA
Haaland abeba tuzo ya PFA
Read also