Na mwandishi wetu
Beki wa kushoto, Adeyum Saleh ameondoka Geita Gold baada ya kudumu kwenye kikosi hicho kwa msimu mmoja na kutimkia Dodoma Jiji.
Uongozi wa Dodoma umemtambulisha rasmi leo mchezaji huyo kupitia kurasa zao za mitandao ya kijamii wakieleza imani yao juu ya mchezaji huyo anayemudu pia nafasi ya winga wa kushoto.
Baada ya kukamilisha dili hilo, Adeyum alieleza namna gani anawashukuru Geita kwa muda wote aliodumu kwenye timu hiyo, akiwatakia kila la heri kwenye michuano wanayoshiriki.
“Alhamdulilah nawashukuru sana viongozi wa Geita pamoja na benchi la ufundi na wachezaji wenzangu pamoja na mashabiki wote, nawatakia kila la heri Inshaalah kwenye mapambano yao, Mungu akipenda tutaonana siku nyingine,” alisema Adeyum.
Adeyum aliyewahi kuzitumikia Simba, Yanga, Coastal Union, Kagera Sugar na nyingine anakuwa mchezaji wa tatu katika dirisha hili dogo la usajili kuondoka Geita baada ya Saido Ntibazonkiza aliyesajiliwa Simba na Yusuph Kagoma anayeelezwa kuvunja mkataba ili ajiunge na Singida Big Stars.
Soka Adeyum atimkia Dodoma Jiji
Adeyum atimkia Dodoma Jiji
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
