Na mwandishi wetu
Nyota wa kikosi cha Yanga waliokuwa na timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars wanatarajia kuungana na wenzao kesho Jumatano kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu NBC dhidi ya Kagera Sugar utakaochezwa Februari 2, mwaka huu.
Wachezaji hao ni Dickson Job, Mudathir Yahya, Ibrahim Hamad ‘Bacca’ na nahodha Bakari Mwamnyeto, mwingine ni Kennedy Musonda ambaye alikuwa na timu ya taifa ya Zambia maarufu Chipolopolo.
Meneja wa Yanga, Walter Harrison alisema leo Jumanne kuwa wachezaji hao walipewa mapumziko ya siku mbili baada ya kurejea nchini wakitokea Ivory Coast na watakuwa sehemu ya msafara utakaokwenda Bukoba kwa ajili ya mchezo wa Kagera.
“Kwa kuwa ratiba imebana, kocha Gamondi (Miguel), aliwapa nyota wote waliokuwa timu za taifa siku mbili za kupumzika kabla ya kujiunga na timu kesho kwa ajili ya safari ya Bukoba ya mchezo wetu wa kiporo dhidi ya Kagera,” alisema Walter.
Meneja huyo alisema baada ya nyota hao, sasa wamesalia wachezaji wawili; kipa Djigui Diarra wa Mali na kiungo mshambuliaji wa Burkina Faso, Stephan Aziz Ki ili kutimiza idadi ya wachezaji saba ambao waliiwakilisha timu zao katika michuano ya Afcon.
Soka Mastaa Yanga kambini Jumatano
Mastaa Yanga kambini Jumatano
Read also