Na mwandishi wetu
Kocha mkuu wa Mtibwa Sugar, Zubeir Katwila amesema timu hiyo haitashuka daraja licha ya kuwa nafasi ya mwisho kwenye msimamo wa Ligi Kuu NBC kwa sasa inayoshirikisha jumla ya timu 16.
Akizungumza na GreenSports leo Jumamosi, Katwila alisema idadi ya mechi zilizobaki na tofauti ya pointi chache kutoka timu moja kwenda nyingi ndivyo vinavyompa matumaini hayo ya kuibakisha kwenye ligi Mtibwa.
“Mtibwa haiwezi kushuka daraja licha ya kwamba tupo nafasi ya mwisho, tuna mechi 10 ambazo mpango wetu ni kushinda robo tatu na hilo linawezekana sababu kwa sasa tumeimarika tofauti na ilivyokuwa awali lakini timu nyingi zimetofautiana pointi chache,” alisema Katwila.
Kocha huyo alisema yeye ni mzoefu sana na ligi ya Tanzania kwa kucheza lakini na kufundisha hivyo bado anaipa nafasi ya kuendelea kushiriki ligi kuu msimu ujao timu yake na si kushuka daraja kama watu wanavyodhani.
Katwila alikiri kuwepo kwa ushindani mkali wakati huu ligi inapoelekea ukingoni lakini watapambana na kuhakikisha lengo lao linatimia.
Mtibwa ipo nafasi ya mwisho kwenye msimamo ikikusanya pointi 16 katika michezo 20 iliyocheza msimu huu, ili isalie ligi kuu msimu ujao inalazimika kupata angalau pointi 20 ili kukaa nafasi salama.
Soka Katwila: Mtibwa haishuki daraja
Katwila: Mtibwa haishuki daraja
Read also