Na mwandishi wetu
Hatimaye klabu ya Simba imekuwa ya kwanza kuweka wazi usajili wake wa dirisha dogo kwa kumtambulisha kiungo mshambuliaji, Saidi Ntibazonkiza kutoka Geita Gold.
Kupitia taarifa waliyoiweka leo, Simba imefafanua kuwa imempa mkataba wa mwaka mmoja na nusu mchezaji huyo raia wa Burundi.
Mapema baada ya kukamilika kwa dili hilo, mchezaji huyo akaelekea Mwanza kujiungana na kikosi kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya mchezo wao dhidi ya KMC utakaopigwa jijini humo kwenye Uwanja wa CCM Kirumba.
Simba imeshawishika kumsajili mchezaji huyo kutokana na kiwango alichokionesha msimu huu akiwa na Geita baada ya kufunga mabao manne na kutoa pasi za mabao sita akizidiwa pasi tatu na kinara Clatous Chama wa Simba.
Aidha, taarifa ya Wekundu hao imeeleza kuwa wanaamini uzoefu wa Ntibazonkiza utaongeza chachu ya ubunifu kwenye safu ya ushambuliaji inayoongozwa na Moses Phiri aliyefunga mabao 10 mpaka sasa akishika nafasi ya pili nyuma ya Fiston Mayele wa Yanga aliyefunga mabao 13.
Ntibazonkiza ambaye amewahi kukipiga MS Caen ya Ufaransa, FC Kaysar ya Uturuki, MKS Cracovia (Poland) na kwingineko alitua mara ya kwanza Tanzania akisajiliwa na Yanga msimu wa 2020/21 akitokea Vital’O ya Burundi kabla ya kujiunga na Geita msimu huu.
Soka Simba rasmi yamsajili Ntibazonkiza
Simba rasmi yamsajili Ntibazonkiza
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
