Na mwandishi wetu
Kocha Mkuu wa Geita Gold, Fred Minziro ameeleza ni kiasi gani anavutiwa na uwezo wa beki wa kulia wa timu hiyo, David Kameta ‘Duchu’ akidai kwua anatamani kuendelea kuwa naye msimu ujao.
Duchu yupo Geita kwa mkopo akitokea Simba, msimu huu ameonesha uwezo mkubwa chini ya Minziro na kuisaidia timu hiyo kushika nafasi ya tano mpaka sasa kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya NBC ikipambana kumaliza nafasi nne za juu.
Minziro ameeleza kuthamini uwezo wa kijana huyo, nidhamu, uelewa wake, mabadiliko yake kiuchezaji ndiyo maana anatamani awe miongoni mwa wachezaji wake kuelekea kwenye vita nyingine ya msimu ujao.
“Ni kijana mzuri kwa kweli, amekuwa na matatizo yake madogo madogo lakini anabadilika kila siku, muelewa, uwezo mkubwa anaonesha, ana nidhamu na kwa kweli niseme ana mchango mkubwa ndani ya kikosi.
“Siwezi kusema lolote kwa sasa lakini ni mchezaji ambaye sidhani kama kuna timu atakwenda atashindwa kucheza au kukosa nafasi moja kwa moja, ni mchezaji mzuri lakini tusubiri wakati wa usajili nao ufanye kazi yake,” alisema Minziro.
Hata hivyo, duru mbalimbali za michezo zinafafanua kuwa Simba haina mpango wa kumrejesha kikosini mchezaji huyo waliyemsajili kutoka Lipuli, hivyo Geita wanaweza kuwa na njia nyeupe kulikamilisha hilo.
Soka Minziro humwambii kitu kwa Duchu
Minziro humwambii kitu kwa Duchu
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
