Barcelona, Hispania
Kiungo wa Barcelona na timu ya Taifa ya Uholanzi, Frenkie de Jong inadaiwa kwa sasa anatamani kujiunga na klabu ya Man United katika kipindi cha usajili majira ya kiangazi baadaye mwaka huu baada ya mpango huo kukwama mwaka jana.
Kabla ya kuanza kwa msimu huu, mchezaji huyo alikuwa akihusishwa na mipango ya kujiunga na timu hiyo huku kocha wa Man United, Eric ten Hag akiwa mstari wa mbele katika mpango huo akitamani kuungana na mchezaji huyo ambaye amewahi kuwa naye katika klabu ya Ajax ya Uholanzi akiamini ana uwezo wa kuibeba timu hiyo.
Katika kipindi hicho, Barcelona walionekana kuwa tayari kumruhusu mchezaji huyo aondoke kutokana na hali ngumu ya kiuchumi iliyokuwa ikiwakabili lakini habari za ndani zilidai kwamba dau kubwa ambalo klabu hiyo ilitaka lilionekana kukwamisha mpango huo.
Kinachoonekana kwa sasa ni kwamba mpango huo unaweza kufanikiwa kwa kuwa mchezaji mwenyewe anadaiwa kutamani kuungana na Ten Hag kwa mara nyingine huku akiamini wakati umefika kwake kupata changamoto mpya katika timu nyingine.
Kwa upande mwingine haijaweza kujulikana kama Ten Hag bado ana nia ile ile ya kumtaka mchezaji huyo kwani wakati mbio za kumsaka De Jong zikiendelea, kocha huyo alifanikiwa kumsajili Casemiro, kiungo wa Brazil aliyekuwa akiichezea klabu ya Real Madrid na ambaye tayari amekuwa na mchango mkubwa katika timu hiyo.
Man United kwa sasa inaonekana kuwa katika mwenendo mzuri ikiwa nafasi ya nne kwenye Ligi Kuu England na ingawa habari ya De Jong haijazungumzwa kwa muda mrefu lakini habari za ndani katika klabu hiyo zinadai kwamba Ten Hag anasaka mchezaji wa kuchukua nafasi ya Cristiano Ronaldo aliyevunja mkataba na timu hiyo na tayari amesajiliwa na klabu ya Al Nassr ya Saudi Arabia.
Kimataifa De Jong aitamani Man United
De Jong aitamani Man United
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
