Barcelona, Hispania
Rais wa klabu ya Barcelona, Joan Laporta amesema kwamba kiungo Frenkie de Jong anataka kubaki katika klabu hiyo licha ya Man Utd kumsaka kwa udi na uvumba.
Man Utd inadaiwa kuwa tayari kutoa Pauni 63.5 milioni ili kumpata kiungo huyo Mholanzi lakini hawajafanikiwa licha ya msaada mkubwa kutoka kwa kocha wa timu hiyo, Erik ten Hag ambaye ni Mholanzia na amewahi kuwa na De Jong katika klabu ya Ajax ya Uholanzi.
Katika hatua ambayo inaonekana ni kuitoa Man Utd katika mpango huo, Laporta anasema kuhusu kungo huyo ambaye ndio kwanza ana miaka 25, “De Jong ni mchezaji wa Barca wa kiwango cha juu na tunataka abaki hapa, ana ofa nyingi lakini tunataka abaki na yeye anataka kubaki.”
De Jong pia amekuwa akihusishwa na mipango ya kutua Chelsea ingawa ni Man Utd ambao wamekuwa wakimuwinda kwa muda mrefu huku ikidaiwa Ten Gag ambaye jana aliuanza vibaya msimu wake wa kwanza katika Ligi Kuu England kwa kichapo cha mabao 2-1 mbele ya Brighton, ndiye aliyeshikilia msimamo wa kumtaka mchezaji huyo kwa takriban miezi mitatu sasa licha ya ugumu uliopo.
Habari za ndani hata hivyo zinadai kwamba licha ya Laporta kujinasibu kuhusu De Jong lakini klabu yake inadaiwa kutaka kumpunguzia mshahara mchezaji huyo kama anataka kubaki katika klabu hiyo ambayo inapitia kipindi kigumu kiuchumi.
Klabu hiyo pamoja na kuwa na hali ngumu kiuchumi lakini tayari imetumia zaidi ya Pauni 120 milioni kwa ajili ya usajili wa Jules Kounde, Robert Lewandowski, na Raphinha huku ikidaiwa kuwa mbioni kumsajili beki wa kushoto wa Chelsea, Marcos Alonso.
Katika kukabiliana na hali ngumu ya kiuchmi Barcelona inatafuta pesa za usajili kwa kuuza haki zao za matangazo ya ndani ya televisheni pamoja na kuuza hisa za kampuni yao ya matangazo ya Barca Studios.
Kimataifa Laporta ambakisha De Jong Barca
Laporta ambakisha De Jong Barca
Read also
