Na mwandishi wetu
Beki wa Simba, Henock Inonga ambaye kwa sasa ni majeruhi, amejumuishwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya DR Congo kinachojiandaa na michezo miwili ya kirafiki dhidi ya New Zealand na Angola.
Inonga amejumuishwa kwenye kikosi hicho cha wachezaji 26 kinachoundwa na kundi kubwa la nyota wanaocheza soka la kulipwa nje ya Afrika lakini imestaajabisha kuona kocha wa timu hiyo, Sebastien Desabre akiwatema nyota wa Brentford ya England, Yoane Wissa na Jordan Ikoko wa Pafos ya Cyprus.
Inonga alipata majeraha katika mchezo wa Ligi Kuu NBC dhidi ya Coastal Union wiki mbili zilizopita na kushindwa kuitumikia timu hiyo katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Power Dynamos ya Zambia.
Wachezaji wengine waliojumuishwa kwenye kikosi hicho ni makipa Lionel Mpasi, Dimitry Bertaud na Baggio Siadi wakati mabeki ni Brian Bayeye, Gedeon Kalulu, Dylan Batubinska, Inonga, Chancel Mbemba, Arthur Masuaku, Rocky Bushiri na Joris Kayembe.
Eneo la kiungo, kuna Aaron Tshibola, Edo Kayembe, Samuel Moutousammy, Elia Meschack, Joel Kakuta, William Balikwisha, Theo Bongonda, Charles Pickel na Grady Diangana.
Na Washambuliaji walioitwa ni Fiston Mayele, Bakambu, Jackson Muleka, Ben Malango, Silas Katompa na Simon Banza.
Kimataifa Majeruhi Inonga aitwa timu ya taifa
Majeruhi Inonga aitwa timu ya taifa
Read also