London, England
Mpango wa bilionea wa Marekani mwenye asili ya Iran, Jahm Najafi kutaka kuinunua klabu ya Tottenham Hotspur umegonga mwamba baada ya wamiliki wa klabu hiyo kusema hawana mpango wa kuiuza.
Najafi (pichani) licha ya kutowasilisha maombi rasmi ya kutaka kuinunua Tottenhamu lakini alidaiwa kutenga kitita cha Pauni bilioni 3.7 lakini wamiliki wameibuka wakidai hawana mpango wa kuiuza.
Badala yake wamiliki hao wamedai wanaifanyia kazi mipango ya muda mrefu ya Spurs na hivyo kufuta mpango wa Najafi ambaye pia ni mmiliki wa kampuni ya uwekezaji katika michezo ya MSP Capital.
Najafi inadaiwa aliingia shauku ya kuinunua klabu hiyo baada ya baadhi ya mashabiki mwezi uliopita kujitokeza na kuwalalamikia wamiliki wa sasa kwa kutowekeza kwa kiasi kikubwa kwenye klabu hiyo.
Taarifa za hivi karibuni za kimahesabu zilieleza kuwa uwekezaji katika klabu hiyo kwa upande wa timu ya wanaume ulifikia kiasi cha Pauni 500 milioni kuanzia mwaka 2019 wakati Chelsea kwenye dirisha la usajili Januari pekee ilitumia Pauni 280 milioni.
Kimataifa Wamiliki Spurs wadai klabu haiuzwi
Wamiliki Spurs wadai klabu haiuzwi
Read also