Na mwandishi wetu
Klabu ya Azam imekuwa miongoni mwa timu za kwanza kutangaza wachezaji wanaoachana nao kwenye dirisha dogo la usajili baada ya leo kutangaza kuachana na kiungo mshambuliaji, Ibrahim Ajibu.
Ajibu ameondoka katika timu hiyo baada ya kukamilika kwa muda wa mwaka mmoja wa mkataba wake tangu atue Azam akitokea Simba katika usajili wa dirisha dogo msimu uliopita, ukiwa ni maalum kwa ajili ya kuziba nafasi ya Aboubakar Salum ‘Sure Boy’ aliyetimkia Yanga wakati wa dirisha hilo.
Azam imetoa taarifa ya kuachana na Ajibu kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram huku ikimshukuru kwa huduma yake tangu ajiunge na timu hiyo ambayo hakufanikiwa kuonesha kiwango cha juu kama ilivyotarajiwa na weng na kwa baadhi ya wachambuzi ilionekana kama mchezaji huyo alijizamisha kwa kuichagua Azam.
Hata hivyo, duru mbalimbali zinaripoti kuwa mchezaji huyo yupo mbioni kujiunga na Singida Big Stars iliyo chini ya kocha Hans van Pluijm kwa ajili ya kukiongezea nguvu kikosi hicho huku taarifa nyingine zikifafanua kuwa tayari amemalizana na walima alizeti hao.
Soka Azam, Ajibu waachana
Azam, Ajibu waachana
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
