Na mwandishi wetu
Klabu ya Mtibwa Sugar imemtangaza Habib Kondo kuwa kocha wao mkuu baada ya kuachana na Salum Mayanga.
Ofisa Habari wa Mtibwa, Thobias Kifaru alisema Kondo anachukua nafasi ya Mayanga ambaye waliachana naye baada ya kumalizika msimu uliopita kutokana na mwenendo mbovu wa timu hiyo.
“Ni kweli tumemchukua Habibu na alianza majukumu yake tangu Julai 18. Tuna imani naye maana ni kijana wetu kwani aliwahi kucheza Mtibwa msimu wa 2001 hadi 2002.
“Walikuwepo makocha wengi walioomba kazi hii ila lengo letu lilikuwa ni kupata kocha mzawa, Habibu ndiye amepita kati ya hao wote na atapewa majukumu yote ikiwemo usajili maana anaifahamu Mtibwa Sugar na anafuatilia ligi,” alisema Kifaru.
Kondo ambaye amewahi kuzifundisha Mbeya Kwanza na KMC FC amepewa fursa ya kuendelea kuunda kikosi cha ushindani msimu ujao, timu hiyo ikitaka kurejesha makali yake iliyokuwa nayo misimu michache nyuma.
Soka Rasmi, Habib Kondo akabidhiwa Mtibwa
Rasmi, Habib Kondo akabidhiwa Mtibwa
Read also
