Na mwandishi wetu
Bondia Mfaume Mfaume, ameshindwa kuhudhuria zoezi la vipimo vya afya leo kuelekea pambano lake dhidi ya Iddy Pialali la kwenye Usiku wa Mabingwa linalotarajiwa kupigwa Desemba 26, mwaka huu.
Pambano hilo la raundi 10 linatarajiwa kuchezwa kwenye ukumbi wa kimataifa wa AICC jijini Arusha.
Kutokana hilo, Pialali ametamba kuwa Mfaume amemuogopa ndiyo maana amechelewa kutokea katika zoezi hilo la upimaji afya lililofanyika Kawe, Dar es Salaam.
“Mfaume hajiamini ndio maana hajatokea, anachotakiwa kufanya ni kuamini tu mazoezi,” alisema Pialali huku akijinadi kuwa amefanya maandalizi mazuri kuhakikisha anafanya vizuri.
“Mimi najigamba halafu nakupiga kweli, nina uhakika wa kazi yangu, nimejipanga vizuri na kiafya niko vizuri namwambia Mfaume nitamfanya kitu kibaya,”alisema.
Mabondia wengine akiwamo Karim Mandonga, alitamba kuwa bondia atakayekutana naye lazima avumilie kwani kipigo alichomwandalia ni ngumi mpya aina ya pelesu pelesu.
Mbali na Mfaume ambaye alichelewa katika zoezi la kupima afya, mabondia zaidi ya 10 wamefanikiwa kupima afya tayari kwa maandalizi ya mwisho kuelekea usiku wa mapambano hayo.
Mratibu wa pambano hilo, Bakari Khatibu alisema wamekamilisha zoezi la kwanza kwa upimaji afya za mabondia kuelekea kwenye pambano hilo ambalo linasubiriwa kwa hamu na mashabiki wa mchezo huo.
Ngumi Mfaume Mfaume ashindwa kupima afya
Mfaume Mfaume ashindwa kupima afya
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
