Manchester, England
Kesi ya kupanga mikakati ya kubaka na shambulio la kimwili iliyokuwa ikimkabili mshambuliaji wa Man United, Mason Greenwood hatimaye imefutwa.
Greenwood mwenye umri wa miaka 21 alikamatwa Januari mwaka jana akituhumiwa kwa kosa la kupanga mipango ya kubaka, tabia za kibabe na udhalilishaji mwili.
Katika taarifa yake Greenwood ambaye Desemba, 2021 alikuwa akiwindwa na klabu za Barcelona na Arsenal, alisema kwamba anajisikia faraja na kuishukuru familia, marafiki na wapendwa wote ambao wamekuwa naye pamoja wakimpa ushirikiano katika kadhia iliyokuwa ikimkabili.
Taarifa ya kimahakama ilidai kuziarifu pande zote husika juu ya uamuzi huo na kwamba wakati wote ilishauriwa kwa mtu yeyote aliyekutwa na kadhia hiyo kujitokeza na kuripoti polisi na uchunguzi ungefanywa kadri ambavyo ingewezekana.
Tangu kuhusishwa na tuhuma hizo, Greenwood alisimamishwa kuichezea Man United lakini baada ya hukumu kutoka, mwakilishi wa klabu hiyo alisema kwamba wamepokea uamuzi wa waendesha mashtaka wa kufuta tuhuma zote zilizokuwa zikimkabili mchezaji huyo.
Kwa mujibu wa mwakilishi huyo hata hivyo, klabu itapitia taratibu zake za ndani kabla ya kuamua hatua zinazofuata, “kwa sasa hatutoweza kusema lolote zaidi ya hilo, ni hadi taratibu zetu zitakapokamilika.”
Kimataifa Greenwood wa Man Utd afutiwa kesi ya ubakaji
Greenwood wa Man Utd afutiwa kesi ya ubakaji
Read also