London, England
Nyota wa zamani wa Arsenal, Martin Keown amesema anashindwa kumuelewa kocha Mikel Arteta kwa kitendo chake cha kukubali kumuondoka, Pierre-Emerick Aubameyang, mchezaji ambaye Keown anasema angekuwa Harry Kane wa Arsenal.
Matatizo ya kinidhamu yalidaiwa kumuandama Aubameyang akiwa Arsenal na kujikuta akiporwa unahodha wa timu hiyo kabla ya kucheza mechi yake ya mwisho katika klabu hiyo, Desemba mwaka jana dhidi ya Everton na hatimaye kutimkia Barcelona.
Mtu wa kwanza kumlaumu Arteta kwa uamuzi huo alikuwa ni beki wa zamani wa timu hiyo, Sokratis Papastathopoulos ambaye alisema kwamba anadhani uamuzi huo haukuwa sahihi na sasa Keown anasema kwamba anadhani Arteta alitakiwa kuendelea kuwa na Aubameyang katika klabu hiyo.
Akifafanua Keown alisema, :Nafikiri alikuwa na sababu za kumuondoa ambazo ni za muda mfupi lakini mwisho wa siku iliathiri timu kwa sababu Arsenal haikuwa ikipata mabao mengi.”
“Ni kweli kwamba unatakiwa kuiheshimu hadhi ya klabu ya soka lakini bado kulikuwa na uhitaji wa kuwamo kwenye Ligi ya Mabingwa mbele ya Spurs. Yule (Aubameyang) ni Harry Kane wetu.
“Nafikiri ni uamuzi mpana wa kocha na bado tuko katika safari ya kuona kama aliloamua litafanya kazi, labda tungembakisha hadi mwisho wa msimu, kwa sasa Jesus (Gabriel) amepata nafasi na Aubameyang anabaki kuwa historia, lakini magoli ni mengi ambayo Arsenal wameyakosa, bado yako katika fikra zangu, nafikiri mchezaji (Aubameyang) angeweza kusamehewa.
Kimataifa Keown ashangaa Arteta kumtema Aubameyang
Keown ashangaa Arteta kumtema Aubameyang
Read also