Na mwandishi wetu
Tanzania imeendelea kung’ang’ania kwenye nafasi ya 119 kwa ubora wa viwango vya Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) vilivyotolewa leo Alhamisi huku ikikamata nafasi ya 32 kwa ubora Afrika.
Viwango hivyo vimekuja baada ya Tanzania kucheza mechi mbili tangu Fifa ilipotangaza viwango vya soka mara ya mwisho miezi miwili iliyopita.
Hivi karibuni timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars ilifungwa na Bulgaria bao 1-0 kabla ya kuichapa Mongolia mabao 3-0 katika michuano ya Fifa Series iliyofanyika Azerbaijan.
Katika viwango hivyo kwa Afrika, Morocco imeendelea kuwa namba moja na ya 13 duniani huku Senegal ikishika namba mbili, ikifuatiwa na Nigeria, Misri, Ivory Coast, Tunisia, Algeria, Mali, Cameroon na Afrika Kusini inakamilisha kumi bora Afrika.
Bingwa wa Kombe la Dunia, Argentina imeendelea kukaa kileleni kidunia ikifuatiwa na Ufaransa inayoshika nafasi ya pili na baada ya hapo zinafuaa nchi za Ubelgiji, England, Brazil, Ureno, Uholanzi, Hispania, Italia na Croatia inayokamilisha 10 bora duniani.
Kimataifa Tanzania yabaki nafasi ya 119 Fifa
Tanzania yabaki nafasi ya 119 Fifa
Read also
