Na mwandishi wetu
Azam FC leo Ijumaa itakuwa kibaruani dhidi ya Bahir Dar Kenema ya Ethiopia kwenye mchezo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho Afrika, ikiapa kulipa kisasi cha kufungwa mabao 2-1 kwenye mechi ya awali.
Kwenye mchezo huo wa mkondo wa kwanza wa raundi ya awali ya michuano hiyo, Azam ilikubali kichapo cha mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Abebe Bikila, Addis Ababa.
Azam inahitaji ushindi wa bao 1-0 na kuendelea ili kufuzu hatua ya kwanza ya michuano hiyo ambapo wakipenya watakutana na Club Africain ya Tunisia.
Kuelekea mchezo huo utakaopigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex kuanzia majira ya saa 1.00 jioni, Azam itaingia na kauli mbiu ya ‘La Revancha’, wakitumia lugha ya Kihispaniola kwa maana ya kulipa kisasi cha kuifunga timu hiyo.
“Maandalizi yote yamekamilika leo, timu iko tayari kwa mchezo, tumejiandaa vya kutosha na dhumuni letu kubwa ni kulipa kisasi cha kufungwa ugenini, na wao tuwafunge hapa kwetu tusonge hatua inayofuata, hilo ndio lengo kubwa mbele yetu,” alisema Ofisa Habari wa Azam, Thabiti Zakaria.
Kimataifa Azam kazini kulipa kisasi
Azam kazini kulipa kisasi
Read also