Na mwandishi wetu
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limepiga marufuku kukusanya, kurekodi, kuchambua na kusambaza data za soka zinazotokana na mechi zilizo chini ya shirikisho hilo.
Taarifa ya TFF iliyopatikana Alhamisi Aprili 30, 2026 ilidai kubaini baadhi ya watu na taasisi ambazo zinajihusisha na usambazaji na ukusanyaji wa data za mechi zikiwamo takwimu bila idhini.
TFF imewakumbusha watu hao kuwa shirikisho hilo tayari lina mshirika wa data ambaye ni Kampuni ya Beta TQ ambayo ndiyo yenye haki ya kukusanya na kusambaza data hizo.
Katika taarifa hiyo TFF imemtaka mtu au taasisi yoyote inayotaka kusambaza data hizo iwasiliane na Kampuni ya Beta TQ ili kupata kibali na ruhusa ya kufanya hivyo.
TFF imetangaza kuwa itakuwa tayari kumchukulia hatua za kisheria yeyote atakayebainika kukusanya data moja kwa moja uwanjani, kutumia wafanyakazi au vifaa vya kufuatilia mechi.
Katazo hilo la TFF pia linamhusu yeyote atakayejihusisha na usambazaji, uuzaji au uchapishaji wa data zisizo rasmi atachukuliwa hatua za kisheria.
Soka ‘Marufuku kusambaza data mechi za TFF’
‘Marufuku kusambaza data mechi za TFF’
Read also
