Na mwandishi wetu
Kocha Mkuu mpya wa KMC, Abdihamid Moallin (pichani) ameeleza kuwa atapambana kuhakikisha anafanikisha ndoto za timu hiyo za kuwa miongoni mwa timu kubwa shindani kwenye soka la Tanzania.
Moallin aliyetambulishwa kuchukua nafasi ya Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ amesema anafahamu ndoto za KMC na anafahamu si rahisi kuzifanikisha ndani ya ligi ngumu kama ya Tanzania lakini atahakikisha analitekeleza hilo.
“Nashukuru Mungu kwa nafasi hii, pia nawashukuru wote kwa kunipa fursa hii na kuniamini kuiongoza klabu hii na ni kitu maalum kwangu, ni changamoto pia kuja hapa sababu napaswa kufanya juhudi zote kuipa mafanikio timu.
“Ligi hii ni ngumu si nyepesi na kilichofanya nije KMC ni mahitaji ya klabu, naamini timu ina ndoto kubwa ya kuwa mshindani wa kweli kwenye mpira wa Tanzania na hii ilitosha kunifanya nikubali changamoto ya namna hii,” alisema Moallin.
Kabla ya kutua KMC, Moallin alikuwa kocha mkuu wa Azam ambayo kwa sasa inaolewa na Youssouph Dabo raia wa Senegal.
Soka Moallin aahidi kupigania ndoto za KMC
Moallin aahidi kupigania ndoto za KMC
Read also