na mwandishi wetu
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetoa ufafanuzi na kueleza kwamba
si vyema kuyashushamashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika kwani yana hadhi na heshima kubwa.
Hayo yameelezwa siku moja baada ya Msemaji wa Yanga, Haji Manara kudai
kuwa mashindano hayo niya watu wanaoshindwa na wala si makubwa kama ambavyo imekuwa
yakielezwa na watu wa soka.
Simba ndiyo timu pekee ya Tanzania iliyokuwa ikishiriki michuano hiyo
kabla ya juzi kutolewa hatua ya robo fainali na Orlando Pirates kwa
mikwaju ya penalti 4-3 hivyo ni kama vile Manara alikuwa akiinanga
Simba.
Mkurugenzi wa Habari na Masoko TFF, Boniface Wambura ameeleza kuwa
kauli hiyo si njema hasa inapotoka kwa mtu wa familia ya soka, hivyo
kama Shirikisho wataangalia kwa kina suala hilo ambalo alikiri ni
kuishushia heshima michuano yenyewe.
“Michuano hii ni mikubwa na imekuwa ikishindaniwa kwa mfumo ambao
unafahamika na mshindi huwa anatafutwa kwa ajili ya kushiriki michuano
hii, mfano mshindi wa Kombe la FA kwa nchi ndiyo anakwenda kushiriki
michuano hiyo kwa ngazi ya Afrika.
“Sasa maana yake unaanza kuushusha au kuudharau mchakato huu kuanzia
kwa shirikisho la nchi. Si sawa kwa mtu wa familia ya soka kuzungumza
mambo kama haya ambayo hayana ukweli wowote zaidi ya kudhoofisha au
kufifisha juhudi za soka kwa ujumla,” alisema Wambura.
Soka TFF yamjibu Manara ishu ya Simba
TFF yamjibu Manara ishu ya Simba
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
