Na mwandishi wetu
Wakati Yanga ikiendelea na mazoezi ya kujifua kwa ajili ya msimu ujao, beki wa kati wa timu hiyo, Bakari Mwamnyeto amekiri ndani ya kikosi hicho kumekuwa na ushindani mkubwa kila nafasi akiamini kocha wa timu hiyo, Nasredine Nabi atakuwa na kazi kubwa.
Mwamnyeto amewasili juzi katika kambi ya timu hiyo, Avic Town iliyoko Kigamboni akitokea kwenye majukumu ya timu ya taifa, Taifa Stars iliyokuwa na mechi za kufuzu kushiriki michuano ya Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN).
Akifafanua kuhusu hali hiyo, Mwamnyeto alisema kuwa imetokana na kuongezeka wachezaji wale waliokuwepo awali na uwepo wa wachezaji wapya mahiri waliosajiliwa na timu hiyo hivi karibuni.
“Kwa sasa kumekuwa na wakati mgumu kidogo kwa sababu wachezaji wote kwa sasa ni wazuri na kila mchezaji anaonyesha kwamba anataka kucheza kwa hiyo sisi kama wachezaji tunafanya majukumu yetu ya kujiweka vizuri zaidi, kazi kwake mwalimu nani ataanza nani atakaa benchi, si kazi yetu tunamwachia mwalimu,” alisema Mwamnyeto.
Yanga ambao ni mabingwa wapya wa Ligi Kuu NBC Bara na Kombe la FA, ilimaliza ligi bila kupoteza mchezo ikiwa na kikosi imara na sasa imeongeza wachezaji wapya Stephane Aziz Ki, Joyce Lomalisa, Lazarous Kambole, Gael Bigirimana na Bernard Morrison wanaotajwa kuwa moto wa kuotea mbali kutokana na viwango wanavyoendelea kuonyesha.
Soka Mwamnyeto azungumzia vita ya namba Yanga
Mwamnyeto azungumzia vita ya namba Yanga
Read also